NEWS

Nyumba ya Baba Meja kunta yavunjwa baada ya kufariki

Download | Play Now
Nyumba ya Baba Meja kunta yavunjwa baada ya kufariki

Nyumba ya Baba Meja kunta yavunjwa baada ya kufariki

Msanii wa Singeli, Meja Kunta amesema kifo cha Baba yake, Mwarami Mtumbuka kimemuachia maumivu makubwa akidai kuwa kwa muda mrefu marehemu alipitia migogoro ya mali, msongo wa mawazo na presha, hali ambayo anaamini ilichangia kuzorota kwa afya yake.

SOMA HII>>>Najua Haulijui Hili La Marehemu Steven Kanumba na Diamond Platnumz

Kupitia ukurasa wake wa Instagram leo Julai 26, 2026, Meja Kunta amesema ameapa kusimamia haki ya Baba yake kwa njia za kisheria na kwa amani, akisisitiza hatapambana kwa chuki wala visasi, bali kwa ukweli na haki, huku akiwataka wote wanaohusika kuwajibika kwa matendo yao mbele ya Sheria.

Aidha, amesema ataomba usikivu na msaada kutoka Serikalini chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ili haki itendeke, akieleza kuwa ana imani atavuka kipindi hiki kwa msaada wa Mungu.

Meja Kunta pia amedai kuwa baada ya kifo cha Baba yake aliumizwa zaidi na matukio yaliyofuata, akisema siku ya pili nyumba ilivunjwa kwa lengo la kutafutwa hati za mali, ambapo amesema hata wakati wa mazishi kulisikika kauli za “tushindane.”

Hata hivyo, amesema ameamua kuyaachia yote kwa Mungu na hatashindana na mtu yeyote, bali atafuata njia za kisheria katika kutafuta haki. Baba wa Meja Kunta, Mwarami Mtumbuka, alifariki dunia Julai 21, 2026 na kuzikwa Julai 22, 2026 katika makaburi ya Kisutu, Jijini Dar es salaam.