Ads 0

Type Here to Get Search Results !

Kesi ya Ronaldo kuanza kuchunguzwa


Mamlaka ya Polisi katika mji wa Las Vegas nchini Marekani imethibitisha kuanza mchakato wa kuchunguza kesi ya mwanadada, Kathryn Mayorga (34) aliyedaiwa kubakwa na staa wa klabu ya Juventus, Cristiano Ronaldo miaka tisa iliyopita.

Katika taarifa iliyotolewa na mamlaka hiyo Jumatatu ya wiki hii, imeeleza kuwa inaifahamu kesi hiyo iliyoripotiwa kutokea 13, June 2009 ambapo katika kipindi hicho ripoti inachukuliwa mwanadada  huyo hakuwaeleza maafisa wa polisi mahali gani tukio lilipotokea.

" Maafisa wetu wanaendelea kufuatilia taarifa zilizotolewa na mlalamikaji. Huu ni uchunguzi unaoendelea na hakuna taarifa zaidi zinazoweza kutolewa kwa sasa ", imesema taarifa hiyo.

Taarifa ambazo mlalamikaji amewaeleza maafisa wa polisi zinadai kwamba baada ya tukio hilo alipokea kiasi cha Pauni 28,7000 ambazo ni sawa na takribani Shilingi 850 millioni za Kitanzania kutoka kwa Ronaldo na kusainishwa mkataba wa kutozungumzia suala hilo mahali popote.

Cristiano Ronaldo (33) mwenyewe amekanusha taarifa hiyo na kuiita ni ya uongo na kwamba mwanadada huyo ana lengo la kumchafua na kujipatia umaarufu kupitia jina lake.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad

Ads 2