Ads 0

Type Here to Get Search Results !

NECTA YATANGAZA MATOKEO DARASA LA SABA, YATAZAME HAPA


BARAZA la Mitihani la Taifa (NECTA) limetangaza matokeo ya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi (darasa la saba) kwa mwaka 2018 ambapo matokeo yanaonyesha ongezeko la ufaulu kwa asilimia 4.76% tofauti na ufaulu wa 2017 ambao ulikuwa asilimia 72.76%

Akitangaza matokeo hayo, Katibu Mkuu wa Baraza hilo, Dkt. Charles Msonde, amesema katika tathmini ya awali kiwango cha ufaulu kimepanda kwa asilimia 4.9% ikilinganishwa na 2017, amesema pia kiwango cha ufaulu wa somo la Kiingereza uko chini sana tofauti na masomo mengine (50%).

NECTA pia limewafutia matokeo watahiniwa 357 waliobainika kufanya udanganyifu kwenye mitihani iliyofanyika mwaka huu 2018.

“Baraza limezuia kutoa matokeo ya watahiniwa zaidi 100 kutokana na kuugua kipindi cha mtihani na kuwapa fursa ya kufanya mtihani huo mwaka 2019,” amesema Msonde.

Kutazama matokeo hayo

Bofya hapa === >Matokeo Darasa la Saba 2018 (Link 1)

Bofya hapa === >Matokeo Darasa la Saba 2018 (Link 2)




JIUNGE NASI KUPITIA YOUBE -NGOMBOZI TV....Bonyeza Subscribe kisha kengele HAPO UTAKUA WAKWANZA KUPATA UJUMBE PINDI HABARI ZETU ZITAKAPORUSHWA HEWANI.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad

Ads 2