About

About
Hii ni tovuti ya kitanzania inayoendeshea shughuli zake nchini Tanzania chini ya usimamizi wa NGOMBOZI MEDIA COMPANY . Tovuti hii inakupa fursa ya kujua na kupakua nyimbo mpya na za zamani za Bongo flava, India, pamoja na Filamu . Yapo mengi kuhusu burudani kwa ujumla utakapotembelea www.ngombozi.com . Haiishii hapo tovuti hii kadri siku zinavyozidi kusonga mbele ndio inazidi kuboresha huduma zake na kuzisogeza karibu. Imani ya wengi inawapelekea kuamini kuwa umakini unaoonyesha hivi sasa na timu ya usimamizi wa tovuti hii utaifanya izidi kuwa maarufu huku ikisogeza huduma karibu na wateja hasa wapenda burudani ya muziki wanaopendelea sana matumizi ya mtandao. Kwa ufupi kabisa hiyo ndiyo Ngombozi media Tovuti ya muziki inayoendeshea huduma zake nchini Tanzania.

Dont Miss

Chanzo Cha Tanzania Kukosa Internet Ya Mitandao Yote May 2024

Chanzo Cha Tanzania Kukosa Internet Ya Mitandao Yote May 2024
Share it:

Shirika la Uchunguzi la Mtandao la NetBlocks limesema changamoto ya ukosefu wa mtandao wa internet imezikumbuka Nchi mbalimbali za Afrika Mashariki na maeneo jirani baada ya nyaya za chini ya bahari kuharibika ambapo imesema Tanzania ndio imeathirika zaidi na hitilafu hiyo pamoja na kisiwa cha Ufaransa cha Mayotte.

Netblocks imesema nyaya za mawasiliano za chini ya habari za SEACOM na EASSy zimeharibika kutokana na hitilafu hiyo ambapo Msumbiji na Malawi wamepata athari kwa wastani huku tatizo hilo likitatuliwa Kenya ambao wameendelea kutumia internet kama kawaida. 

Nchi nyingine zilizoathirika ni Burundi, Somalia, Rwanda, Uganda, Madagascar na Visiwa vya Comoros ambazo nazo zilipata shida ya changamoto ya internet kwa kiasi cha chini.


Share it:

Fresh Air

NEWS

Post A Comment:

0 comments: