Simba Sc Washusha Mbadala wa Chama Jr
Tayari Joshua Mutale Kiraka wa Zambia ameshatambulishwa rasmi Msimbazi, jana mchana ilikuwa zamu ya Steve Mukwala Staa wa Uganda.Lakini sasa unaambiwa Simba imetuma tiketi mbili za ndege katika mataifa mawili tofauti ili kuwashusha nchini wachezaji wawili matata akiwemo mrithi wa Clatous Chama aliyetangazwa kujiunga na Yanga Juzi.
Kati ya tiketi hizo moja imeenda Kinshasa DR Congo kwa winga Elie Mpanzu ambaye niliripoti dili lake kitambo sana na nyingine imetumwa Abidjan Ivory Coast kwa kiungo mshambuliaji Jean Charles Ahoua (22) anayetazamiwa kuwa mrithi wa Chama pale msimbazi.
Msimu uliopita aliibuka mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Ivory Coast tuzo ambayo msimu uliopita ilishikiliwa na Pacome Zouzoua na msimu mmoja nyuma aliibeba Stephane Aziz Ki na wote sasa wanacheza Yanga. Katika msimu huo, Ahoua alifunga mabao 12 na kutoa pasi za mwisho 6.
Post A Comment:
0 comments: