MATOKEO Yanga Vs Al Hilal Leo Tarehe 26 November 2024Matokeo ya kufungwa mabao 2-0 nyumbani kutoka kwa Al Hilal kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, yameendeleza mkosi ambao Yanga imekuwa nao kwenye mechi za mwanzo za hatua ya makundi ya mashindano ya klabu Afrika.Mabao ya Adama Coulibaly katika dakika ya 63 na Yasir Mozamil katika dakika ya 90 ya mechi ya leo, yameifanya Yanga kutowahi kupata ushindi kwenye hatua ya makundi ya mashindano ya klabu Afrika, mara zote sita ambazo imewahi kushiriki.Mara ya kwanza kwa Yanga kushiriki hatua hiyo ilikuwa ni mwaka 1998 ilipotinga katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo mechi ya kwanza, Yanga ilitoka sare ya bao 1-1 nyumbani na Manning Rangers ya Afrika Kusini.
No comments