BAAB KUBWA: Rayvanny Achafua Trending Kwa Kasi ya Ajabu
Staa wa muziki wa Bongo Flava maarufu kama Rayvanny amegeuza jina la wimbo wa “Tetema” kuwa “brand” inayozalisha rekodi kila inapoguswa. Ndani ya siku nne tu, ameweka rekodi mpya kwenye YouTube Music kwa kufikisha monthly audience milioni 10.9, akimpita Boss wake wa zamani, Diamond Platnumz aliyewahi kushikilia rekodi ya milioni 10.2. Wasikilizaji wa Rayvanny wameongezeka kutoka milioni 4.88 ndani ya siku tatu tu, Hizi ni zaidi ya namba kwa Muziki wa Msanii Rayvanny.
RELATED: Rayvanny Ft Nora Fatehi, Shreya Ghoshal - Oh! Mama Tetema
Toka Ujio wa Oh Mama! Tetema akishirikiana na Mwanamuziki Nora Fatehi, Vishal Mishra na Shreya Ghoshal umepokelewa kama keki mpya iliyotoka jikoni, kila mtu anataka kipande chake. Video yake ilitazamwa zaidi ya mara milioni 7.4 ndani ya saa 24 za kwanza pekee, ikiongoza karibu dunia nzima.
Huu ni uhalisia wa jinsi muziki wa Tanzania (Bongo Flava) unavyozidi kupenya kimataifa. Rayvanny ameonyesha kwamba remix sahihi inaweza kuchanganya tamaduni na mashabiki wa aina tofauti mbili duniani hadi kuleta mlipuko wa namba kwenye majukwaa yote. Hata Spotify, monthly listeners wake wamepaa kutoka 403,900 hadi 603,700 ndani ya siku 4 tu.
Kwa ukuaji huu, na ambavyo ‘Oh Mama Tetema’ inaendelea, Rayvanny anaweza kumaliza mwezi Agosti akiwa na wasikilizaji wa YouTube zaidi ya milioni 20 akiweka rekodi nyingine kubwa zaidi.
Kifupi, Tetema imegeuka injini ya rekodi, na Rayvanny ndiye dereva wa mashindano haya ya muziki wake duniani.

No comments