Neno Lake La Kwanza Baada ya Kupona Afya Ya Akili
Ebitoke Kupitia ukurasa wake Wa Instagram Ameandika Haya:
Ningependa kuchukua nafasi hii kuwashukuru kwa moyo mmoja mashabiki wangu wote NA KILA MMOJA ALIEGUSWA kwa upendo wenu mkubwa, maombi yenu ya dhati, na sapoti yenu ya hali ya juu wakati nilipokuwa napitia kipindi wakati nilipokua Napitia Changamoto ya AFYA YA AKILI ILIYOSABABISHWA NA KULOGWA .
Kila ujumbe, kila sala, na kila neno la faraja mlilolituma lilinigusa sana na kunitia moyo. Nimehisi uwepo wenu kwa karibu hata katika MAOMBI YENU, na hilo halijapita bila mimi kutambua.
Kwa sasa, naendelea vizuri kwa neema ya Mungu, na nafsi yangu imejaa shukrani kwa jinsi mlivyokuwa nami kwa njia ya kipekee. Asanteni kwa kunionesha kwamba upendo wa kweli bado upo.
Naendelea kupona na kurudi katika hali yangu ya kawaida, nikiwa na matumaini mapya na nguvu mpya yote hii ni kwa sababu yenu pia. Mbarikiwe sana kwa wema wenu.

No comments