Hii Hapa Ratiba na Tarehe ya Mazishi ya Mchekeshaji Mc Pilipili
Mwili wa Emmanuel Mathias, maarufu MC Pilipili utazikwa Novemba 20,2025 jijini Dodoma familia imeeleza.
Hayo yameelezwa leo Jumatatu Novemba 17,2025 na Mratibu wa Mazishi hayo MC John Mwangata aliyesema kila kitu kwa ajili ya mazishi hayo kimeshaaandaliwa.
MC Pilipili alifariki jana Jumapili Novemba 16,2025 jioni ikiwa ni muda mfupi kabla ya kwenda kuongoza sherehe.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, Dk Ernest Ibenzi alithibitisha jana kuwa mwili wa mshereheshaji huyo ulipelekwa hospitalini hapo na wasamaria wema kati ya saa 10.30 hadi saa 11 jioni.
Mapema leo dada wa MC Pilipili, Veronika Mathias alisema bado hawajapanga taratibu za maziko kwani walikuwa wakimsubiri kaka yao mkubwa anayeishi jijini Dar es Salaam.
“Familia imeshapanga kuwa ndugu yetu MC Pilipili tutamuweka katika nyumba yake ya milele siku ya Alhamisi ya Novemba 20,2025, naomba tuendelee kuwa wapole na tuzidi kutoa michango yetu kama tunavyotakiwa,” amesema MC Mwangata.

No comments