Breaking News

Msanii Christian Bella Apewa Uraia Wa Tanzania

Msanii Christian Bella Apewa Uraia Wa Tanzania
Msanii maarufu wa muziki Afro-pop, wenye ladha ya kibongofleva Christian Bella Obama (CBO) hatimaye amepewa uraia wa Tanzania baada ya kuishi kwa miaka zaidi ya 20 akifanya muziki hapa nchini. Bella ambaye amekuja Tanzania akiwa na miaka 17 mpaka sasa ana miaka zaidi ya 30 amefunguka kuwa..

 “Nashukuru M/Mungu, Nashukuru serikali ya Tanzania na watanzania kwa Ujumla, Watanzania wananipenda na watanzania Ndio wamenibeba, nina miaka 20 ndani ya Tanzania, Niliingia nikiwa na miaka 17 ilikuwa under 18.”
 “Kufanya kazi nchi ambayo haujazaliwa sio kazi ndogo, lakini Nimekuja nikiwa mdogo nimepokelewa vizuri, kitu inaonesha napendwa sana sihitaji kuwa na nyimbo MPYA ili kupewa kazi, napata kazi sana kuliko wasanii waliopo kwenye trending” 
“Sijapewa uraia kwa Sababu nina watoto na Mtanzania ni process ndefu sana na lazima kuzifuata hata kama unapendwa na viongozi,  nilifuata utaratibu sio Kwamba Bella kapewa kirahisi, na utaratibu sio mrahisi ni kazi ndefu sana, inaanzia serikali za mitaa unakuja Wilayani, unaenda kwa Mkuu mkoa, kuna vitu vingi, na ukiwa mgeni lazima uoneshe ulikuwa unaishi halali.. hawatoi uraia Sababu Bella unaimba vizuri Hapana, hata ukifanya miaka 40, lazima ufuate process, nimekaguliwa vitu vingi sana, kuna Polisi na vitu vingi sana” Amefunguka Bella 

Hata hivyo uraia wa Bella umetangazwa Na Waziri wa  Mambo ya Ndani, George Simbachawene Mapema Wiki Hii, Desemba 18, 2025 siku ya wahamaji duniani. ambapo waziri Simbachawene amesema Tanzania kuna idadi kubwa ya wahamiaji na baadhi yao wamekuwa wakipewa uraia. Hapo mwanzo Bella alikuwa raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ambaye ameishi Tanzania kwa muda mrefu akifanya shughuli za kisanii.

No comments