About

About
Hii ni tovuti ya kitanzania inayoendeshea shughuli zake nchini Tanzania chini ya usimamizi wa NGOMBOZI MEDIA COMPANY . Tovuti hii inakupa fursa ya kujua na kupakua nyimbo mpya na za zamani za Bongo flava, India, pamoja na Filamu . Yapo mengi kuhusu burudani kwa ujumla utakapotembelea www.ngombozi.com . Haiishii hapo tovuti hii kadri siku zinavyozidi kusonga mbele ndio inazidi kuboresha huduma zake na kuzisogeza karibu. Imani ya wengi inawapelekea kuamini kuwa umakini unaoonyesha hivi sasa na timu ya usimamizi wa tovuti hii utaifanya izidi kuwa maarufu huku ikisogeza huduma karibu na wateja hasa wapenda burudani ya muziki wanaopendelea sana matumizi ya mtandao. Kwa ufupi kabisa hiyo ndiyo Ngombozi media Tovuti ya muziki inayoendeshea huduma zake nchini Tanzania.

Mourinho awataja wasaliti wake katika klabu ambao ni hawa

Mourinho awataja wasaliti wake katika klabu ambao ni hawa
Share it:
Meneja wa Manchester United Jose Mourinho anasema baadhi ya wachezaji wanajali zaidi, baada ya klabu hiyo kukosa kushinda katika mechi tatu za karibuni zaidi walizocheza. katika mechi mbili za majuzi zaidi walizocheza United ligini, walitoka sare na Wolves lakini wakashindwa na West Ham.Kwa sasa wameshuka hadi nafasi ya 10 kwenye Jedwali la Ligi ya Premia.
Aidha, walitupwa nje ya klabu ya Derby kutoka michuano ya Kombe la Carabao. Alipoulizwa kama ana wasiwasi kuhusu kazi yake iwapo klabu hiyo itaendelea kuandikisha matokeo mabaya, Mourinho alijibu: “La hasha.”
Mourinho alikuwa akizungumza kabla ya United kukutana na Valencia lao katika mechi ya hatua ya makundi Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya. “Kila mchezaji ni tofauti, wachezaji hawafananai,” alisema. “Naviona vitendo tofauti, lakini kile unachoona si kile kilichomo ndani.
“Huwa naona kwamba nawakera watu, baadhi ya watu ambao huwa hawaonekani ni kama wameshindwa kwenye mechi. “Naona hivi hivi, lakini katika vikao viwili vya mazoezi tulivyokuwa navyo (tangu Jumamosi) kila kitu kilikuwa kawaida, hamu ya kutaka kutia bidii na kucheza.”
Mourinho aliongeza: “Kile ninachoweza kukifanya kuboresha mambo huwa nakitenda, na nitaboresha mambo ambayo yananitegemea mimi na kazi yangu.”
Kushindwa 3-1 na West Ham Jumamosi ilikuwa mara ya tatu kwa United kushindwa mechi ya Ligi ya Premia katika mechi saba walizocheza mwanzo wa msimu huu.
Aidha, ndio mwanzo mbaya zaidi wa msimu kwao tangu 1989-90. Mourinho alipoulizwa iwapo amezungumza na kaimu mwenyekiti mtendaji wa Manchester United Ed Woodward tangu washindwe na West Ham alisema: “Hilo ni jambo la faragha. Sijawauliza nyinyi huwa mnazungumza na nani. Hilo ni jambo la siri.”
Kiungo wa kati wa United Nemanja Matic alicheza katika mechi hiyo ambayo walishindwa na West Ham, uchezaji ambao beki Luke Shaw alisema ulikuwa wa kusikitisha. Matic aliongeza: “unapocheza na Manchester United, kila mtu hutarajia kwamba utashinda mechi.”
“Unapokosa kushinda mechi mbili mtawalia, unaelekezewa macho zaidi – tunajua hilo.
“Mechi hiyo ilikuwa mbaya sana. Sifikiri kuna mchezaji yeyote ambaye huingia uwanjani na kukosa kujaribu (kushinda)”.
Akizungumzia tamko la Shaw, Mourinho alisema: “Anasema ‘sisi ni wachezaji uwanjani, ni lazima tucheze vyema, ni lazima tujitume’.
“Naufurahia mtazamo huo lakini sikubaliani naye kabisa. Ni sisi sote, kila mtu katika klabu hii ana mchango wa kutekeleza.
“Tunaposhinda tunashinda sote. Tunaposhindwa, tunashindwa sote. Na tunaposhindwa, lawama ni kwa kila mtu.”
Mourinho anataka kufutwa?
Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal na England Ian Wright anasema taarifa hasi ambazo zimekuwa zikienea kuhusu Manchester United ni za aibu.
Wright aliambia BBC kwamba: “Ni kama jambo linalotokea kila siku. [Mourinho] huzungumza kuhusu baadhi ya wachezaji kujali zaidi ya wengine, lakini huwa hawataji kwa majina – mbona useme hivyo basi? “Labda anataka kutufumba macho tuache kuangazia kwamba hii ndiyo changamoto kubwa zaidi amewahi kukumbatana nayo, kujaribu kuboresha mambo. “Inaaibisha kwa Manchester United. Wasimamizi wa klabu wanafanya nini? Haya yataendelea hadi lini?”
Mshambuliaji wa zamani wa Norwich na Blackburn Chris Sutton amesema ni wakati wa Mourinho kuondoka. “Nashuku kwamba mwenyewe anataka afutwe,” anasema Sutton. “Ni mtu mjanja. Angependaje basi kuendelea na kuendelea kwa kuwa na uchokozi?”
Msimu huu, Mreno huyo amezozana na karibu kila mtu Old Trafford.
  • 29 Julai: Mourinho v aliwazomea mashabiki
  • 29 JulaiMourinho v Ed Woodward – kuhusu ununuzi wa wachezaji
  • 10 Agostit: Woodward v Mourinho – alipozuiwa kuwasajili mabeki
  • 28 Agosti: Mourinho v wanahabari – alisema anastahili heshima
  • 1 Septemba: Mourinho v Anthony Martial – alisema yuko radhi Mfaransa huyo andoke
  • 24 Septemba: Paul Pogba v Mourinho Sura ya 1- Pogba azozana naye kwa kukosoa mbinu za klabu waliposhindwa na Wolves
  • 25 SeptembaMourinho v Pogba Sura ya 2 – Apokonya Pogba unahodha
  • 26 Septemba: Mourinho v Pogba Sura ya 3 – Waonyesha wazi uhasama mazoezini
Chanzo BBC
Share it:

Michezo

Post A Comment:

0 comments: