Breaking News

Mohamed Salah Ameachwa Na Klabu Ya Liverpool

Mohamed Salah Ameachwa Na Klabu Ya Liverpool
Timu ya Liverpool imemuacha mshambuliaji wake Mohamed Salah kuelekea mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL) dhidi ya Inter Milan utakaopigwa leo Jumanne Desemba 9,2025.... 
Ambapo klabu hiyo inaamini kuwa kuachwa kwa nyota huyo raia wa Misri kwa sasa ni kwa manufaa ya pande zote kufuatia maelewano mabovu na kocha Arne Slot.. 
Hatua hiyo inakuja siku mbili tu baada ya kufanya mahojiano yaliyozua sintofahamu akidai klabu hiyo imeamua kumbebesha mzigo wa lawama kufuatia mwenendo usioridhisha wa klabu hiyo akikaa benchi kwenye mechi tatu mfululizo. 

Katika mahojiano hayo Salah pia alidai uhusiano wake na kocha Arne Slot umevunjika na kwamba mechi ya Jumamosi dhidi ya Brighton huenda ikawa mechi yake ya mwisho Anfield. Inaelezwa uamuzi wa kuachwa kwa Salah ni wa klabu kwa mashauriano na kocha Slot.

No comments