Rapa Tekashi 6ix9ine Ahukumiwa Tena Miezi 3 Jela
Msanii wa Hiphop Tekashi 6ix9ine amehukumiwa kifungo cha miezi mitatu jela baada ya kupatikana na hatia ya kukiuka masharti ya supervised release aliyopewa kufuatia kesi yake ya awali ya makosa ya shirikisho.....
Kwa mujibu wa taarifa mpya kutoka vyanzo vya kuaminika, zinaeleza kuwa rapa huyo "Daniel Hernandez" alikiri makosa na alijisalimisha katika Kituo cha Metropolitan Detention Center huko Brooklyn tarehe6 Januari.....
Hii itakuwa ni mara yake ya pili kwenda jela ndani ya kipindi cha mwaka mmoja. Mnamo Novemba 2024, 6ix9ine alihudumia kifungo cha wiki sita baada ya kukiri makosa kadhaa ya kuvunja masharti ya uangalizi, ikiwa ni pamoja na safari zisizoidhinishwa kwenda Las Vegas na Sarasota, pamoja na kufeli vipimo vya matumizi ya dawa za kulevya mara mbili na kupatikana na athari za methamphetamine.
Hukumu hii mpya imeibua mjadala mpana kuhusu tabia ya msanii huyo na uwezo wake wa kufuata masharti ya kisheria, hasa baada ya kupewa nafasi mara kadhaa lakini kuendelea kufanya makosa yanayokiuka masharti ya mahakama.

No comments